Tuimarike Pamoja: Kuimarisha Jamii za Waathiriwa ili Kumaliza Ukatili wa Kingono wa Utotoni.

Tangazo la Maombi

Utangulizi

Licha ya dhamira ya kila nchi kumaliza ukatili dhidi ya watoto, hali hii inazidi kuongezeka kote duniani. Ingawa kuna jitihada kubwa za kilimwengu zilizofanywa ili kupambana na ukatili, mara nyingi jitihada hizi zinashindwa kujiungamanisha na uhalisia wa kila siku unaowakabili watoto na vijana wanaopitia ukatili. Matukio mengi ya ukatili wa kingono dhidi ya watoto (kuanzia hapa itajulikana CSV) hayaripotiwi kutokana na mapengo katika mifumo ya ulinzi na utekelezaji wa sheria, ikiwemo pia unyanyapaa na mila potovu za kijamii zilizo hasi, kuhusiana na ukatili wa kingono.  

Lakini, watu ambao wamepitia matukio ya CSV pamoja na washirika wao, wanaelewa kabisa uhalisi uliopo, wana habari chungu nzima na wana utaalamu unaotokana na uzoefu wa kuchangia ili kuzuia na kuitikia aina hiyo ya ukatili. Inasikitisha kwamba kumekuwa na fursa chache za msaada wa kifedha katika kusaidia jitihada zao za uongozi.

Ignite Philanthropy: Kuhamasisha Kumaliza Ukatili Dhidi ya Wasichana na Wavulana ilianzishwa na Taasisi za Human Dignity, Oak, na Mfuko wa Hisani wa Wellspring ili kuimarisha matokeo katika kuzuia aina zote za ukatili dhidi ya watoto. Kwa kushirikiana na Taasisi ya Oak, taasisi ya Ignite Philanthropy inazindua programu ya utafutaji ufadhili na ujengaji uwezo ya Tuimarike Pamoja. Programu hii inalenga kuongeza jitihada za maandalizi na mashirika ya kijamii yanayoongozwa na watu waliopitia uzoefu na washirika wao wa karibu.  Ignite Philanthropy inafadhiliwa na Mfuko wa New Venture Fund.

Tuimarike Pamoja ni nini?

Tuimarike Pamoja ni programu iliyoundwa kupambana na CSV kwa kuwawezesha waathiries pamoja na washirika wao kushughulikia mambo ya msingi yanayofanya aina hii ya ukatili kuendelea. Ili kukabiliana na hili suala, Tuimarike Pamoja inalenga kuwekeza kwenye mashirika, kuimarisha uwezo wao wa pamoja na binafsi, kutanua mtandao wao katika harakati pana zaidi zinazoshugulikia kumaliza ukatili dhidi ya watoto (SVAC), na kuondoa vikwazo vyovyote vinavyozuia athari yake.

Tumepanga kuitekelezaje?

Programu inatoa ruzuku 10 za thamani ya $20,000 kwa mwaka mmoja ili kusaidia kukiwepo uwezekano wa kuongeza muda bila gharama zozote kwa hadi miaka miwili kama ikibidi. Mashirika yanayounga mkono kazi zinazolenga uzoefu ambao watu wamepitia wanaweza kutumia fedha hizi kadri wanavyoona inafaa, ikiwa miradi yao inalingana na kanuni muhimu za programu, ambazo zinajumuisha: 

  • Kuonyesha uelewa wa mahitaji ya watu walioathirika na CSV katika mazingira ya eneo lao.

  • Kutumia fedha ili kuimarisha jitihada zao za pamoja/za kishirika katika kukabiliana na CSV.

  • Utayari wa kushiriki uelewa wao na mambo waliyojifunza pamoja na watu wengine katika suala hili, kwa njia ambazo zinalingana na kusudi na maono yao ambayo timu ya Ignite itatoa fursa na kuwezesha miunganiko.

  • Kutoa kipaumbele kwa usalama na matunzo ya wafanyakazi/watu wanaojitolea na kila mtu anayehusika katika kazi zao

Nani anaweza kutuma maombi?

Programu inakaribisha maombi kutoka kwenye mashirika yaliyosajiliwa na mashirika yasiyosajiliwa. Wanufaika wa ufadhili ambao hawajasajiliwa watafadhiliwa kupitia taasisi mshirika iliyosajiliwa. Wakati wa mchakato wa uteuzi, maelezo zaidi na fomu zitatolewa kwa vikundi vilivyofuzu. 

Unahimizwa kutuma maombi endapo shirika lako linatimiza vigezo vifuatavyo:

  • Mnashiriki kikamilifu katika kuzuia au kupambana na unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto na kushughulikia mambo yanayosababisha ukatili huo, kwa kuzingatia muktadha mahsusi na mahitaji ya jamii zilizoathirika.

  • Nyinyi ni shirika lisilosajiliwa linalojiendesha lenyewe, linalojumuisha angalau watu watatu au asasi ya kiraia ambayo kwa pamoja hufanya maamuzi. Tafadhali kumbuka kuwa kama shirika lisilosajiliwa, unaweza kufadhiliwa kupitia washirika waliosajiliwa tu.

  • Nyinyi ni kikundi au asasi ya kiraia isiyosajiliwa ambayo imeundwa, imeundwa kwa pamoja, inaongozwa, au inaongozwa kwa pamoja, na watu waliopitia uzoefu wa matukio ya CSV.

  • Kwa sasa hampokei msaada muhimu kutoka Taasisi ya Oak wala hampati kiwango kikubwa cha fedha za msaada, iwe ni moja kwa moja au kupitia mfadhili wa kati.

  • Kwa sasa hampokei msaada muhimu kutoka Taasisi ya Oak wala hampati kiwango kikubwa cha fedha za msaada, iwe ni moja kwa moja au kupitia mfadhili wa kati.

Tunafadhili maeneo gani?

Ingawa tunatambua kuwa haya ni masuala yanayoathiri jamii zote duniani, Tuimarike Pamoja (katika awamu yake ya kwanza) ingependa kushughulikia utofauti wa ufadhili uliokwepo kwa kuzindua programu hii katika maeneo mahsusi ambapo kuna fursa chache za ufadhili wa namna hii.    

Kimahususi kabisa tunalenga maeneo ambapo miktadha ya kijamii, uchumi na kisiasa inawaathiri watoto waliopitia ukatili kwa viwango tofauti, kwa kuwapa fursa chache za wao kuweza kukabiliana na sonona na kuishi kwa furaha. Kutokana na hili, programu iko wazi kwa mashirika katika maeneo yafuatayo: Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, Asia Kusini, Afrika iliyo Kusini mwa Jangwa la Sahara, na Ulaya Mashariki.

Tunafadhili nini?

Ufadhili unaweza kutumika kwa chochote ambacho shirika linahitaji kwa kuandaa na kuimarisha uwezo wao, inaweza kuwa mafunzo, huduma za kisaikolojia, vifaa, mishahara, usafiri nk. Mbali na fedha za kufadhili mahitaji ya shirika, mashirika yanayosaidiwa yatakuwa na fursa ya kujifunza, kuboresha uwezo wao wa uendeshaji mashirika, na kushirikisha wengine na kuungana na mashirika mengine yanayoshughulikia CSV ulimwenguni.

Taasisi zinachaguliwaje?

Kanuni kuu ya programu ya Tuimarike Pamoja ni kwamba mchakato mzima, kuanzia muundo wa programu hadi uteuzi wa washirika wa taasisi, utaongozwa na kikundi cha washauri ambao wamepitia uzoefu wa matukio ya ukatili wa ngono na/au wana uzoefu wa maandalizi, utetezi au uanaharakati katika suala hili. Kundi hili linaitwa Jopo la Washauri Waliopitia Uzoefu wa CSV (LEAP)

Kwa hiyo, maamuzi ya mwisho kuhusiana na mashirika/taasisi 10 kuorodheshwa ili kuweza kupata ufadhili wa Tuimarike Pamoja, utang’amuliwa na Jopo la Washauri Waliopitia Uzoefu wa CSV. Wanachama wa LEAP ni wawakilishi wa maeneo mbalimbali ya kijiografia yanayohudumiwa na programu hii. Wanachama wa LEAP watatimiza jukumu muhimu katika kuhakikisha mchakato wa uteuzi ni wa haki na usio na upendeleo.   

Namna ya kutuma maombi?

Ikiwa nyinyi ni shirika lililopo katika moja ya maeneo maalum na kuongozwa au kuongozwa pamoja na watu waliopitia uzoefu katika muktadha wa CSV, tutafurahi kusikia kuhusu simulizi ya shirika lako. Ili kutuma maombi, jaza tu fomu ya maombi mtandaoni au tutumie fomu  katika muundo wa Word (inatolewa na tangazo) kwenda kwa applications@ignitephilanthropy.org hadi ifikapo mwisho wa siku Oktoba 22. Jisikie huru kuwasiliana nasi kupitia barua pepe hii hii endapo utakuwa na maswali au unahitaji msaada zaidi. Maombi yanaweza kuwasilishwa kwa Kiarabu, Kifaransa, Kiingereza, Kirusi na Kiswahili.

Mara tutakapopata maombi yako, kutakuwa na hatua chache katika mchakato wa ufanyaji maamuzi kabla hatujarejea kwako:  

  1. Ukaguzi wa kiusimamizi: Timu ya Ignite itafanya ukaguzi wa awali wa kiutawala ili kuhakikisha kuwa ombi lako linaendana na wigo wa kijiografia na vigezo vya utimilivu masharti ulioainishwa kwenye muswada huu (Novemba).

  2. Ukaguzi wa kiusimamizi: Timu ya Ignite itafanya ukaguzi wa awali wa kiutawala ili kuhakikisha kuwa ombi lako linaendana na wigo wa kijiografia na vigezo vya utimilivu masharti ulioainishwa kwenye muswada huu (Novemba).

  3. Majadiliano na makubaliano: Wanachama wa LEAP watapitia maombi yaliyopokelewa, wakishiriki katika majadiliano ili kuchagua mashirika kumi ambayo yanaweza kuchaguliwa kupokea fedha (Disemba).

  4. Kutangaza uamuzi: Wafanyakazi wa Ignite watawasiliana nawe ili kukueleza kuhusu uamuzi (Disemba).

  5. Wafanyakazi wa Ignite watawasiliana na wahitimu kuwaambia kuhusu uamuzi, na wahitimu wataombwa kutoa taarifa na nyaraka za uthibitisho kwa ajili ya ukaguzi. (Disemba/Januari 2024).

  6. Wahitimu wataambiwa kuhusu uamuzi wa mwisho kuhusu kufaulu kwa ukaguzi wa vithibitisho na watafahamishwa kuhusu maelezo ya mchakato wa malipo. (Januari 2024) 

  7. Mwanzo wa utoaji wa ufadhili unakadiriwa kuwa Januari 2024 na muda utakuwa mwaka mmoja kutoka tarehe ya kuanza.

  8. Kilichobaki ni utekelezaji wa mipango ili shirika lako liimarike.   

*Muda uliotajwa ni makadirio tu na unaweza kubadilika kutokana na wingi wa maombi na mambo tusiyoweza kudhibiti.

Fomu ya Maombi Swahilli